31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Vannesa ammwagia sifa Madam Rita

Vanessa6mdmNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MWIMBAJI wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee, amempa sifa Mkurugenzi wa Bench Mark Production, waandaji wa kipindi cha kuibua vipaji vya muziki cha Bongo Stars Search ‘BSS’, Rita Poulsen ‘Madam Rita’, kuwa ni mwanamke anayestahili kuigwa na wanawake wengi nchini.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Vanessa alisema sifa hizo amezitoa ikiwa ni siku ya kuzaliwa kwa Rita, ambaye kwa kiasi kikubwa ameweza kuibua vipaji vingi vya wasanii wachanga.
Vanessa alisema Rita ni mwanamke aliyeweza kubadilisha maisha ya vijana wengi ambao wamekuwa na ndoto za kufika mbali kimuziki.
“Mara nyingi nimekuwa nikisema Rita ni mwanamke jasiri, nimemuona jinsi gani anavyojituma kuhakikisha maisha ya vijana wenye ndoto za kuwa wanamuziki yanabadilika,” alisema Vannesa.
Alisema anamuheshimu sana mwanadada huyo kwani amekuwa akimshawishi na kumpa moyo wa kufanya mambo yanayomvutia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles