28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Basata kubana wasanii wanaokejeli

Basata shilole1NA MWALI IBRAHIM

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wasanii wanaotumia lugha chafu na ukiukwaji wa maadili hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Katibu mkuu wa baraza hilo, Gofrey Mngereza, alisema baraza hilo litachukua hatua stahiki kwa wimbi la wasanii wanaovunja maadili, wanaokaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi zao za sanaa jambo ambalo linazua malalamiko, masikitiko na hofu kwa mashabiki wa kazi za sanaa.

“Lugha zenye maneno machafu ya matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau na udhalilishaji wa makada wa vyama mbalimbali zimekuwa zikitolewa na wasanii hao kupitia muziki wao wakilenga kuigawa jamii na kufifisha amani, upendo, uzalendo na ustaarabu tulionao Watanzania.

“Ieleweke kwamba kwa mujibu wa misingi ya sanaa duniani kote kazi zote za sanaa zinapaswa zionye, zielimishe, ziadabishe, zikosoe, ziburudishe, zihamasishe na zichochee maendeleo chanya katika jamii na siyo kugawa na kuivuruga jamii,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles