23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Barnaba: Video ya ‘Nakutunza’ itachelewa

barnaba11NA CHRISTOPHER MSEKENA

MKALI wa Bongo Fleva, Elius Barnabas ‘Barnaba’ amesema video ya wimbo wa ‘Nakutunza’ aliomshirikisha nyota kutoka Uganda, Jose Chameleone, itachelewa kutoka kwa sababu ya staa huyo wa Uganda kuzongwa na kazi nyingi.

“Chameleone amebanwa na kazi zake atakapokuwa tayari ndiyo tutafanya video, nafikiri nitafanya nje ya nchi kwa sababu wimbo ni mkubwa na nataka unitangaze vema kimataifa, sitaki kukurupuka, ndiyo maana katika wimbo uliowahi kuumiza kichwa changu ni huu wa ‘Nakutunza’,” alisema Barnaba.

Barnaba alisema wimbo huo utaanza kusikilizwa Alhamisi ya wiki hii kupitia vituo mbalimbali vya redio vya ndani na kisha utachezwa na vituo vya redio vya nje ya nchi na baada ya muda usiojulikana ndipo video yake itafanyika.

“Nimeshakaa na mwandikaji wa miswada ananiandikia mwongozo bora kwa ajili ya video hiyo, sijui itakuwaje kwa kuwa nimeipania sana initangaze ndani na nje na niwe wa kimataifa zaidi, lakini pia Fally Ipupa naye kuna kazi tumepanga kuifanya nafikiri wengi wanajua hilo,’’ alieleza Barnabas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles