28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kili Stars yapangwa kundi la kifo Chalenji

NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) jana limepanga droo ya michuano ya Kombe la Chalenji, itakayoanza Novemba 21 mwaka huu nchini Ethiopia.

Droo hiyo imeonyesha kuwa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, imepangwa kundi A sambamba na wenyeji Ethiopia, Somalia na Zambia ‘Chipolopolo’ iliyoalikwa kwenye michuano hiyo na kulifanya kuwa kundi la kifo.

Wawakilishi wengine wa Tanzania, Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ wenyewe wamepangwa kundi C na Sudan, Sudan Kusini na Rwanda, itayotumia michuano hiyo kunoa makali kujiandaa na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika jijini Kigali mwakani.

Mabingwa watetezi Kenya ‘Harambee Stars’ wamepangwa kundi B, sambamba na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Uganda ‘The Cranes’ waliotwaa kombe hilo mara 13, Burundi na Djibouti.

Kilimanjaro Stars itaingia kwenye kinyang’anyiro hicho mwaka huu ikiwania kubeba taji la nne katika michuano hiyo ambayo mwaka jana haikufanyika kutokana na kukosekana kwa wadhamini.

Mara ya mwisho kutwaa kombe ilikuwa mwaka 2010, michuano hiyo ilipofanyika jijini Dar es Salaam kwa kuifunga timu iliyoalikwa ya Ivory Coast bao 1-0, lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na nahodha wa zamani wa kikosi hicho, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles