26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Barcelona wapata pigo kwa Dembele

BARCELONA, HISPANIA

TIMU ya Barcelona itakosa huduma ya mshambuliaji wao wa pembeni Ousmane Dembele kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja baada ya kusumbuliwa na nyama za paja.

Mchezaji huyo alicheza dakika 90 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliopita ambapo Barcelona ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Athletic Bilbao likifungwa na Aritz Aduriz dakika za lala salama.

Uongozi wa timu hiyo umethibitisha kuwa utaikosa huduma ya mchezaji huyo kwa wiki tano baada ya kuumia mguu wake wa kushoto.

Dembele amekuwa na furaha ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Hispania tangu alipojiunga mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund, lakini mara nyingi anasumbuliwa na majeruhi ya misuli.

Msimu uliopita alipata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara tofauti na Philippe Coutinho, lakini alionekana anakosa umakini uwanjani, wakati huo Coutinho akiachwa benchi kutokana na kuwa chini ya kiwango jambo lililompelekea mchezaji huyo kutolewa kwa mkopo Bayern Munich.

Kuumia kwa Dembele kunaweza kuwafanya Barcelona wapambane kuhakikisha wanaipata saini ya mchezaji wao wa zamani Neymar Jr ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya PSG na pia anawindwa na Real Madrid. Dili hilo linaweza kukamilika kabla ya kufungwa kwa usajili Septemba 2.

Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Hispania, Barcelona ilimkosa mchezaji wao bora duniani Lionel Messi kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Hata hivyo kuna taarifa kwamba anaweza kuwa ndani ya kikosi wakati wa mchezo wa pili dhidi ya Real Betis ambao utapigwa kwenye uwanja wa Camp Nou mwishoni mwa wiki hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles