25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Baraza jipya la mawaziri laiva

pombeNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli, wakati wowote anatarajiwa kutangaza Baraza la Mawaziri baada ya kukamilisha wiki kadhaa za kuchuja majina ya wanaofaa kuwa mawaziri.

Hatua hiyo inakuja baada ya jana kukutana faragha kwa saa moja na Waziri Mkuu wake Kassim Majaliwa katika kikao kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo.

Katika kile kinachoonekana ni tofauti na marais waliopita, ambao wengi wao walikuwa wakifuatwa ofisini, hali imekuwa tofauti kwa Dk. Magufuli ambaye aliamua kwenda ofisini kwa Waziri Mkuu Majaliwa na kufanya naye mazungumzo.

Chanzo chetu cha habari kilipasha kuwa katika mazungumzo hayo kati ya Dk. Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na mambo mengine, walijadili hatua za mwisho za uteuzi wa mawaziri ambao watakuwa tayari kufanya kazi kwa kujituma na wakati wote kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

“Sasa Baraza la Mawaziri limeiva na kikao kati ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa ni hatua ya mwisho kabla ya uteuzi ambapo majina ya walioteuliwa yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

“Mazungumzo yalikuwa marefu kwa muda wa saa moja ambapo pamoja na kuweka mikakati ya Serikali ya awamu ya tano, lakini pia suala la mawaziri lilichukua nafasi kwa wakuu hawa,” alisema mtoa habari wetu.

Rais Magufuli, anatarajiwa kuteua sura nyingi mpya huku baadhi ya mawaziri wa zamani huenda wakaangukia pua kwa kutorudishwa tena kwenye baraza.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa Serikali ya awamu ya tano katika kampeni zake aliahidi kuteua baraza dogo la mawaziri ambalo litakuwa na watu wachache wenye kujituma wakati wote.

Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, 2015 ikiwa na Wizara 30 ambapo alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, aliunda Baraza la Mawaziri na naibu wao 60.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles