22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kadi za Christmas, mwaka mpya marufuku’

sefueNA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa gharama za Serikali kwa mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Balozi Sefue, alielekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.

“Badala yake Balozi Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananchi/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa.

 

Kupiga marufuku uchapishaji wa kadi hizo kunaendelea  kuonyesha utekelezaji wa azma ya Rais John Magufuli ya kubana matumizi ya Serikali kwa kufuta shughuli za Serikali ambazo hazina tija kwa maendeleo.

Katika hotuba yake ya kufungua Bunge la 11 mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Magufuli alitilia mkazo ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni likiwemo suala la kufuta makongamano, sherehe na maazimisho ambayo hufanywa na wizara na taasisi za umma na kugharimu fedha nyingi za serikali.

Rais Magufuli alianza kutekeleza ahadi yake hiyo siku chache baada ya kuapishwa  kwa kufuta safari zote za nje kwa watumishi wa serikali na kutoa masharti kwa yeyote anaytaka kusafiri kuomba kibali maalumu kutoka kwa rais au Katibu Mkuu Kiongozi kwa kueleza umuhimu wa safari yake kwa taifa.

Siku chache baadaye alitangaza kufutwa kwa sherehe za uhuru ambazo hufanyika Disemba 9 kila mwaka na badala yake akaelekeza siku hiyo iadhimishwe kwa watu nchi nzima kufanya usafi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles