20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Barabara ya mwendo kasi yamfikisha kizimbani

Barabara ya mwendoMANENO SELANYIKA NA SABRINA HAMZA (TSJ),DAR ES SALAAM

MKAZI wa Tandika wilayani Temeke, Mohamed Jamal (32), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na makosa ya kuendesha gari katika barabara ya mabasi yaendayo haraka (BRT).

Mbele ya Hakimu Obadia Bwegego, wakili wa Serikali, Nancy Mushumbusi, alidai   kwamba tukio hilo lilitokea Mei 31 mwaka huu barabara ya Morogoro eneo la Ubungo.

“Mtuhumiwa unakabiliwa na kosa la kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kuendesha gari   ya Toyota IST   namba   T.594 CEA, ulitumia barabara ya mabasi yaendayo haraka wakati ukitambua ni kinyume cha sheria,” alidai Mushumbusi.

Mashtaka mengine   ni pamoja na kuendesha gari katika barabara ya umma bila kuwa na leseni wala bima.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana makosa hayo na upelelezi umekamilika hivyo upande wa Serikali uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusoma maelezo ya awali.

Mtuhumiwa aliachiwa huru kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles