Na Mohamed Shaban, Kiteto
Zaidi ya magari 30 likiwamo la Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, Tumaini Magessa yamekwama katika eneo la Twanga, Kata ya Namelock mkoani hapa.
Mkuu wa Wilaya huyo na abiria wengine walikwama barabarani hapo kwa saa kadhaa leo Jumapili Machi 18 ambapo barabara hiyo inatajwa kuwa mbovu na kusababisha uharibifu kwa watumiaji wake mara kwa mara.
Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) namshauri wa masuala ya barabara wilayani humo, Gerald Matindi amekiri eneo hilo kuwa korofi na kuongeza kuwa ujenzi umeanza ambapo wanaotengeneza ni Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Manyara
“Tanroads wako kazini na tayari wameweka vifusi kwa ujenzi huo ingawa bado kuna tatizo la kukwama magari kwa sasa lakini muda si mrefu litaisha,” amesema.