23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BARABARA MBOVU YAMKWAMISHA MKUU WA WILAYA

 

Na Mohamed Shaban, Kiteto


Zaidi ya magari 30 likiwamo la Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, Tumaini Magessa yamekwama katika eneo la Twanga, Kata ya Namelock mkoani hapa.

Mkuu wa Wilaya  huyo na abiria wengine walikwama barabarani hapo kwa saa kadhaa leo Jumapili Machi 18 ambapo barabara hiyo inatajwa kuwa mbovu na kusababisha uharibifu kwa watumiaji wake mara kwa mara.

Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) namshauri wa masuala ya barabara wilayani humo, Gerald Matindi amekiri eneo hilo kuwa korofi na kuongeza kuwa ujenzi umeanza ambapo wanaotengeneza ni Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Manyara

“Tanroads wako kazini na tayari wameweka vifusi kwa ujenzi huo ingawa bado kuna tatizo la kukwama magari kwa sasa lakini muda si mrefu litaisha,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles