24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

ACT-WAZALENDO: LUKUVI SHUGHULIKIA WAWEKEZAJI WANAOPORA ARDHI WANANCHI

Na Mwandishi wetu    |   

Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema kimemwandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuingilia kati ukiukwaji wa sheria unaofanywa na watendaji wa serikali wenye dhamana ya kutekeleza sheria ya ardhi na kutokufanyika kwa mpango bora wa matumizi ya ardhi za vijiji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Machi 18, kuhusu tathmini ya ziara yake katika kata zinazoongozwa na ACT-Wazalendo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema migogoro mingi ya ardhi husababishwa na wanaotajwa kama wawekezaji katika vijiji kugawiwa maeneo ya wananchi ya uzalishaji.

“Aidha uhifadhi umekuwa ukiingilia ardhi za vijiji na kuchukua maeneo makubwa ya vijiji katika baadhi ya vijiji na kusababisha adha kwa wananchi kunyang’anywa ardhi zao, mazao na mifugo huku wakipigwa kwa kisingizio cha kuvamia maeneo ya hifadhi na baadhi yao kutozwa faini kubwa.

“Mifano hai inapatikana katika kata za Mbwawa Kibaha, Tomondo jimbo la Morogoro Kusini, Kata ya Bugaga Kasulu, Msambara Kasulu na Kata ya Buhigwe jimbo la Buhigwe.

“Kutokana na hali hiyo, tumemwandikia Waziri Lukuvi aingilie suala hili”” amesema Zitto.

Zitto amesema licha ya juhudi za Waziri Lukuvi kushughulikia migogoro ya Ardhi, chama chake kinaamini kuwa Serikali kwa kiasi kikubwa inashirikiana na watu wenye fedha kupora ardhi za wananchi wanyonge.

“Serikali itazame upya namna ya kushughulika na migogoro ya ardhi na hasa kuwapa wananchi mashamba pori yote ambayo wawekezaji waliyapora kutoka kwa wananchi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles