28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

‘BANGI’ YA WEMA YAZUA UTATA MAHAKAMANI

BANGI inayodaiwa kukutwa kwa Mlimbwende Wema Sepetu na wenzake wawili imezua utata na kusababisha kesi kuahirishwa baada ya Wakili wake, Tundu Lissu kudai ni vishungi vya sigara.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kutoa uamuzi wa kupokea ama kukataa kielelezo cha bangi anayodaiwa kukutwa nayo mshtakiwa Wema na wenzake Agosti 18, mwaka huu.

Mahakama imefikia uamuzi huo leo Agosti 15, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya bangi hiyo ambayo ni msokoto mmoja na vipisi viwili kupingwa na Wakili wa utetezi Tundu Lissu huku shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima akiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula aliomba kutoa bangi kama kielelezo katika kesi hiyo mahakamani.

Amedai alipima msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi ambapo  ameomba kuitoa bahasha iliyofungwa, yenye muhuri, saini ya shahidi huyo na namba ya maabara 291 ya 2017 mahakamani hapo kwa utambuzi.

Upande wa utetezi haukuwa na pingamizi hivyo bahasha hiyo iliyofungwa ilipokelewa kwa utambuzi na shahidi alidai ndani ya bahasha kulikuwa na msokoto mmoja, vipisi viwili ndani yake vina majani ya bangi na akaomba kuifungua lakini Wakili Lissu alipinga kisipokelewe kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.

“Mheshimiwa hakimu vipisi viwili vyenye majani  ukiviangalia kwa makini ni vishungi vya sigara ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua, kwetu vinaitwa twagooso, kitu kinachoitwa msokoto wa bangi hakijulikani  kimefungwa fungwa  tu karatasi, kuna kibiriti, karatasi nyekundu, haiwezekani vitu vilivyotolewa kwenye bahasha kuwa ndiyo vitu shahidi alivielezea, mahakama isikubali kuvipokea kama kielelezo,” amedai Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Wakati mwingine huwa nashindwa kuelewa pale ambapo wanasheria wanapopingana kwa hoja za kisheria halafu mmojawao anashindwa. Je ni kutokujua sheria au ni kushindwa kujenga hoja au huruma kutoka kwa aliyeshindwa au ni udhaifu wa kiuweledi au ni ukurupukaji wakati wa ukamataji kiasi cha kucha mambo ya msingi yanayoweza kumuweka mtuhumiwa hatiani?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles