26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

‘MSIOSTAHILI HATI ZA DIPLOMASIA RUDISHENI UHAMIAJI’

IDARA ya Uhamiaji  imewataka watu waliopewa hati za kusafiria zenye hadhi kidiplomasia wakati hawastahili kuwa  kuzirudisha katika idara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Agosti 15 na Idara ya Uhusiano ya Uhamiaji, watu wote ambao wamefikia ukomo wa utumishi wa nyadhifa na hadhi hizo, wanatakiwa kurejesha pasipoti hizo kwenye Ofisi za Uhamiaji ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo, kama yalivyo matakwa ya Kifungu cha 8(2) cha Sheria tajwa hapo juu.

“Katika Vifungu Namba 10(2) na (3) na Jedwali la Pili na la Tatu la Sheria hiyo, makundi mbalimbali ya watu wanaostahiki kupewa pasipoti hizo yameainishwa isipokuwa wale ambao kwa mujibu wa nyadhifa zao wanaruhusiwa kisheria kuendelea kutumia Pasipoti hizo hata baada ya kustaafu kwao wakiwemo viongozi wakuu wa nchi wastaafu, wakuu wa mihimili ya dola wastaafu na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wastaafu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu kwenye Sheria,” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na hali hiyo watu hao wametakiwa baada ya kuisha kwa kipindi tajwa yaani mwezi mmoja baada ya kutolewa kwa taarifai, wasiostahiki kuwa nazo watazuiliwa safari zao mara watakapopita katika vituo vya kuingia na kutoka nchini ikiwa ni pamoja na viwanja vya ndege.

Taarifa hiyo ya Uhamiaji ilieleza uwa kuendelea kuwa na Pasipoti hizo kwa wasiostahiki ni kosa kisheria chini ya kifungu cha 19(2)(k) cha Sheria tajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles