27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA LEMA INAYOHUSU UKUTA KUENDELEA LEO

Na JANETH MUSHI- ARUSHA

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, leo imepanga kuanza kusikiliza rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ( Chadema), anayekabiliwa na shtaka la kuhamasisha watu washiriki maandamano ya Ukuta.

Mawakili wanaomwakilisha Lema, waliwasilisha kwa njia ya mdomo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga uamuzi uliotolewa Februari 8 mwaka huu, ambapo mawakili hao walitaka kesi hiyo ikasikilizwe Mahakama ya Katiba (Mahakama Kuu), mbele ya jopo la majaji watatu kutokana na kuwa na masuala ya kikatiba kwenye hati ya mashtaka.

Awali, rufaa hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa Julai 12 mwaka huu mbele ya Dk. Modester Opiyo, lakini ilishindikana baada ya wakili John Mallya anayemtetea Lema, kuieleza mahakama hiyo, kuwa hawajajipanga kwa ajili ya kusikiliza kesi kwa kuwa walijua siku hiyo kesi ilitakiwa kutajwa.

Wakili Mallya aliiomba mahakama hiyo kuahirisha rufaa hiyo na kuipangia tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikiliza ili yeye na mawakili wenzake wa utetezi waweze kuwasilisha hoja zao.

Jaji Dk. Opiyo alikubaliana na ombi hilo la wakili huyo na kuahirisha rufaa hiyo hadi Agosti 16 mwaka huu, saa 4:30 asubuhi itakaposikilizwa.

“Agosti 16 mwaka huu, saa 4:30 asubuhi, mjiandae kwa ajili ya usikilizwaji wa rufaa na siyo kutajwa,” alisema jaji huyo.

Februari 8, mwaka huu, mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ilitoa uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na mawakili wa Lema, katika kesi ya jinai namba 352/2016, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Benard
Nganga, ambaye alitupilia mbali pingamizi hilo na kusema mahakama hiyo ina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles