27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Banana Zoro kusaka vipaji vipya baada ya Ramadhani

Banana Zoro
Banana Zoro

NA JASMIN SEIF,

MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa Rumba, Banana Zoro, amepanga kufanya shindano lenye lengo la kupata wasanii wenye vipaji katika uimbaji, upigaji wa gitaa, kinanda na upulizaji wa tarumbeta.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika mara baada ya mfungo wa Ramadhani kukamilika.

Banana ameliambia MTANZANIA kuwa lengo la kuandaa tamasha hilo ni kuibua na kuendeleza vijana wenye vipaji  hususani wanaotumia mtindo wa Rumba lakini hawajui namna ya kutimiza malengo yao katika muziki.

“Nafasi ndiyo hiyo, vijana wenye ndoto za kuwa kama mimi wajitokeze kwa wingi ili waweze kutimiza lengo lao kupitia vipaji vyao,” alisema Banana.

Akizungumzia mipango yake ya muziki, Banana ambaye pia ni mmiliki wa B Band, anatarajia kuachia albumu yake mpya aliyowashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo, Young D na Young Killer.

Alizitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni ‘Bado kidogo’, ‘Samehe’, ‘Sahau’ aliomshirikisha Young Killer na ‘When she is higher’ aliomshirikisha Young D.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles