27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Mulamula, Waziri wa China wazungumza

Na mwandishi wetu,  Dakar

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi  jijini Dakar nchini Senegal.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea kuridhishwa kwao na ushirikiano na uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na China na kuahidi kuendeleza uhusiano huo kwa faida ya pande zote mbili.

Waziri Mulamula amemhakikishia Waziri Yi utayari wa Serikali  kuendelea kushirikiana na China katika kuhakikisha Tanzania inafikia maendeleo ya kweli kwa ufanisi mkubwa.

Amemshukuru waziri huyo kutokana na ahadi iliyotolewa awali na Rais Xi Jinping wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa FOCAC ya kutoa dozi bilioni moja zaidi za chanjo ya virusi vya Covid 19 kwa Bara la Afrika kwani kitendo hicho kitazisaidia nchi za Afrika kutoa chanjo ya ugonjwa huo kwa watu wengi zaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi na ujumbe wake (kulia) walipokutana kwa mazungumzo jijini Dakar nchini Senegal.

Ameishukuru China kwa kuwa soko la bidhaa za Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania iko tayari kutumia fursa ya soko la China la kuuza mazao yake ya mbogamboga na matunda ili kuongeza ujazo wa biashara na hivyo kukuza uchumi.

Pia ameelezea ambavyo Tanzania inafarijika na utayari wa China katika kuisaidia kmiradi mbalimbali kama ile ya  ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme utokanao na maji kama ya Ruhuji, mradi wa uendelezaji wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji , upanuzi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete  na ujenzi wa barabara kuu katika Visiwa vya  Zanzibar miradi ambayo amesema itasaidia kuinua na kukuza uchumi wa nchi.

Naye Waziri Yi kwa ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono China na kuahidi kuendelea na harakati za kusaidia nchi zinazoendelea na kuongeza kuwa China itaendelea kuisadia Tanzania katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati na kuielezea Reli ya TAZARA kama moja ya kielelezo cha ushirikiano huo.

Amesema China itaendelea kuunga mkono jitihada za Tanzania katika kujikwamua kiuchumi na kuahidi kuendelea kutoa misaada ya fedha na  kitaalamu ili  kukamilisha miradi ya ujenzi, uanzishwaji wa kituo cha mfano kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.

Mawaziri hao wako Senegal kuhudhuria  Mkutano wa Nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika nchini Senegal ulioanza Novemba 29  hadi 30 Novemba  2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles