Balotelli kurudishwa Liverpool

Mario BalotelliMILAN, ITALIA

NYOTA wa Liverpool ambaye anakipiga kwa mkopo katika klabu ya AC Milan, Mario Balotelli, anatarajiwa kurudishwa Liverpool kutokana na kushindwa kuonesha uwezo wake.

Mchezaji huyo tangu amejiunga na klabu hiyo amecheza michezo 20 ya Ligi ya nchini Italia na kufanikiwa kufunga bao moja.

Mmiliki wa klabu ya AC Milan, Silvio Berlusconi, ameweka wazi kwamba kuna wachezaji wanatakiwa kuachwa katika kipindi hiki cha majira ya joto akiwemo Balotelli.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Liverpool lakini mchezaji huyo Aprili mwaka huu aliwahi kusema kwamba hataki kurudi katika klabu hiyo ya nchini England.

“Kuna wachezaji wengi wataondoka katika kipindi hiki cha majira ya joto, Mario Balotelli atakuwa ni miongoni mwa wachezaji hao ambao tutamalizana, wachezaji wengine ambao wataondoka ni pamoja na Philippe Mexes, Alex, Kevin-Prince, Boateng na wengine,” alisema Berlusconi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here