22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo: Soka langu nitalimalizia Madrid

Cristiano RonaldoMADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kwamba hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo hadi atakapotangaza kustaafu soka lake.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2018, lakini mchezaji huyo amedai yupo tayari kuongeza mkataba kama uongozi utakuwa tayari kufanya naye mazungumzo baada ya fainali za Ligi ya Mabingwa.

Inadaiwa kwamba mchezaji huyo anawindwa na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ufaransa, PSG pamoja na klabu yake ya zamani Manchester United.

“Ni wazi kwamba nahitaji kuendelea kuwa hapa, naweza kusema kwamba soka langu nitalimalizia hapa, kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza mkataba baada ya kumalizika kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa, nina furaha kuwa hapa na ninaweza kusema hakuna klabu bora kama hii,” alisema Ronaldo.

Mchezaji huyo amewatoa wasi wasi mashabiki wake baada ya kupata majeraha mazoezini akiwa anajindaa na mchezo huo wa fainali dhidi ya Atletico Madrid ambao utapigwa kesho, mchezaji huyo amesema anaendela vizuri na kuna uwezekano wa kuwepo katika kikosi cha kwanza.

“Nilidhani nitakuwa nimeumia sana, lakini hali yangu kwa sasa ipo vizuri na tutakuwa pamoja katika mchezo wa fainali dhidi ya Atletico Madrid,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles