26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Babu Tale: Tusimsimange Chid Benz mitandaoni

Babu-TaleNA SUZANA MAKORONGO (RCT)

MENEJA wa msanii, Abdul Nassib ‘Diamond Platinum’, Hamisi Tale ‘Babu Tale’, amewataka wadau wa muziki, wasanii na Watanzania kwa ujumla kuacha kumsimanga msanii, Chid Benz ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa ni mambo yanayoweza kumtokea mtu yeyote.

Babu Tale alisema kwa sasa msanii huyo yupo mikono salama chini yake akiwa chini ya uangalizi wa kituo cha Life And Hope Rehabilitation Organization, kilichopo Ukuni huko Bagamoyo akipambana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Babu Tale alisema yeye kama mdau wa muziki wa Bongo Fleva na meneja anasaidia wasanii wengi ili wapate mafanikio kupitia muziki na kwenye matatizo pia anawasaidia.

“Nimechukua jukumu la kumsaidia Chid Benz, naomba Watanzania tumuombee aweze kupona na si kumchafua kupitia mitandao,” alieleza Tale.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles