24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta aanza vema Stars

asteeNA MWANDISHI WETU,

NAHODHA mpya wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’,  Mbwana Sammata, ameanza kuitumikia vema nafasi yake hiyo kwa kuiwezesha Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chad ugenini, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017, uliofanyika katika Uwanja wa Omnisport Idriss Mahamat Ouya, mjini D’jamena.

Kwa matokeo hayo Stars imefikisha jumla ya pointi nne katika Kundi G, ikiwa na timu za Misri, Nigeria na Chad hii ni kutokana na kushinda mechi moja, kutoa sare moja dhidi ya Nigeria (0-0) na kufungwa na Misri (3-0).

Samatta ambaye amerithi mikoba ya nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, aliifungia Stars bao pekee la ushindi katika dakika ya 30 ya pambano hilo akimalizia pasi ndefu ya Farid Musa.

Baada ya bao hilo Stars inayonolewa na mzawa Charles Boniface Mkwasa, ilionekana kucheza kwa uangalifu mkubwa hadi kipindi cha kwanza na kumaliza kipindi cha kwanza wakiongoza 1-0, wakati wenyeji wao wakicheza kwa kujihami ili kutoruhusu kufungwa mabao mengi.

Katika kipindi cha pili timu zote mbili ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini hakuna iliyofanikiwa kuliona lango la mwenzake na kufanya mchezo kumalizika kwa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufufua matumaini ya kufuzu kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika Gabon mwaka 2017.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles