22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Snura: Sitaki mtoto mwingine wa nje ya ndoa

Snura na meneja wake HKNA ESTHER GEORGE

LICHA ya kuwa na watoto wawili kwa baba tofauti, mkali wa kuimba na kunengua, Snura Mushi, amesema kwa sasa hataki apate mtoto mwingine hadi atakapoolewa.

Msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Chura’ alisema wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi hawakuwa na msimamo na mwelekeo anaoutaka hivyo kwa sasa anataka mwanaume mwenye maadili, imani na upendo kwake, kazi yake na familia kwa ujumla.

“Mimi ni mwanamke, nina watoto wawili kwa sasa na ninatamba na wimbo wangu mpya wa ‘Chura’, lazima nitamani kuolewa lakini sitamani kuwa na mtoto mwingine nje ya ndoa, nataka niolewe na mwanaume mwenyewe awe na imani, mapenzi kwangu na kazi yangu kwa ujumla,” aliesema Snura.

Snura aliongeza kwamba anaamini mwanaume akiwa na imani atapenda muziki wake ambayo ndiyo kazi yake, atampenda yeye na familia yake lakini akikosa imani pia hatokuwa na imani naye.

Snura jana alitembelea ofisi za gazeti hili zilizopo Sinza Kijiweni na kuzungumza na waandishi wa habari wa magazeti ya Dimba, Bingwa, Mtanzania, Rai na The African.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles