24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Baba amzuia mwanaye Mbeya City

IMG_0686NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

BABA mzazi wa kipa namba moja wa timu ya Mbeya City, Abdallah David, amemzuia mwanaye David Burhani, kuichezea timu hiyo kwa kile alichodai kupotezewa muda na timu hiyo.

Burhani alisimamishwa kwa muda usiojulikana na uongozi wa timu hiyo, siku chache baada ya kudaiwa kuihujumu timu hiyo katika mchezo wao dhidi ya Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine mjini humo, Yanga walishinda mabao 3-1 huku Burhani akidaiwa kufanya uzembe wa kuruhusu kufungwa bao la pili na mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Burhani alisema kuwa hana mpango wa kuendelea kuitumikia Mbeya City na hiyo imetokana na baba yake kumtaka aachane nayo kwa kuwa imeonekana kuendeshwa kwa fitina.

Alisema baba yake alimtaka kutafuta nafasi ya kucheza sehemu nyingine hata kwenye klabu zisizoshiriki Ligi Kuu ili kuendeleza kipaji chake na yeye hakuona ubaya kwa kuwa mkataba wake unamruhusu kufanya mazungumzo na timu yoyote.

“Kutokana na hali iliyojitokeza, baba amenishauri kutoendelea na Mbeya City, kwani inaonekana kuna watu wachache wenye mamlaka ya kutoa maamuzi kulingana na matakwa yao na si kwaajili ya maendeleo ya timu.

“Sikuona ubaya ushauri wa baba yangu na katika hilo nimeanza mazungumzo na timu kutoka nje ya nchi ambazo zinapakana na Mkoa wa Mbeya, kama mambo yakienda vizuri kuna uwezekano nikaondoka na kwenda kuanza maisha mapya,” alisema.

Akizungumzia juu ya suala lake na uongozi wa Mbeya City, Burhani alisema kuwa hadi sasa hajapokea taarifa yoyote kutoka kwa uongozi wa timu hiyo.

“Waliniambia wanafanya uchunguzi tuhuma zinazonikabili hivyo nitakuwa nje hadi watakapokamilisha suala lao, lakini hadi sasa sijapokea taarifa yoyote kutoka kwao name sioni umuhimu wa kuwauliza,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles