30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Marais wa EAC kujadili sekta ya uchukuzi

Veronica Romwald na Jacqueline Swai (RCT), Dar es Salaam

MARAIS wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mara ya kwanza watakutana nchini kujadili jinsi ya kushirikiana kwa pamoja katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji katika ukanda wa kati (Central Corridor).
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, alisema marais hao watakutana Machi 23, mwaka huu na nchi zitakazoshiriki ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Leo (jana) Makatibu Wakuu wa sekta ya uchukuzi wamekutana na kujadili taarifa za wataalamu wa nchi hizi kwa nia ya kuteua vipaumbele ambavyo vitawasilishwa kwa marais na wao watavijadili na kutoka na kauli moja,” alisema.
Alisema baada ya marais hao kukubaliana vipaumbele hivyo vitakavyowasilishwa Machi 24, mwaka huu watakutana na wawekezaji mbalimbali na kuviwasilisha.
“Marais watatembelea bandari ya Dar es Salaam ambayo imekuwa ikitumika kuingiza mizigo nchini na kisha kusafirishwa kwa nchi washirika ikiwamo Uganda, DRC, Burundi na Rwanda.”
Alisema siku hiyo marais hao watazindua safari tatu za treni za mizigo ambapo moja itakuwa na behewa 20 itabeba mizigo ya DRC, ya pili Rwanda na ya tatu yenye behewa 22 itabeba mizigo ya Uganda.
“Hizi ni safari mpya ambazo zitazinduliwa siku hiyo na niseme kwamba hii si nguvu ya soda, treni hizi zitafanya safari kwa muda wa wiki moja moja nia yetu mizigo yote iondoke bandarini kwa pamoja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles