26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yasubiri mpinzani wa Klabu Bingwa Afrika

AzamNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Azam FC imeanza kupiga hesabu za mbali ikiwaza timu moja kati ya nane zitakazotolewa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ambayo itakutana nayo baada ya kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kimataifa.

Azam imepata matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kutokana na matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 iliyopata dhidi ya timu ngumu ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa awali wa hatua ya 16 bora.

Wawakilishi hao wa Tanzania waliofanikiwa kuitupa nje ya michuano hiyo timu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 7-3 ikiwa ni ushindi wa 3-0 ugenini na 4-3 nyumbani, wanakabiliwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Esperance utakaochezwa Aprili 19, mwaka huu nchini Tunisia.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Dennis Kitambi, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wana matumaini ya kufanya vyema Jumanne ijayo hivyo wameanza kuumiza vichwa kuwaza timu watakayokutana nayo katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), iwapo Azam itasonga mbele itakutana na moja ya timu zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alisema matarajio ya benchi la ufundi ni kuiondosha Esperance katika michuano hiyo jambo ambalo wanaamini linawezekana kutokana na maboresho yaliyofanywa na kocha mkuu wa timu hiyo Mwingereza, Stewart Hall.

“Ni jambo zuri kuanza kuwafikiria wapinzani tutakaowakabili mbeleni ili kupanga mbinu na mikakati mapema, kama inavyofahamika kwamba klabu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni nzuri,” alisema Kitambi.

Wachezaji wa Azam wanatarajiwa kuingia kambini kesho kuanza maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Esperance utakaochezwa mjini Rades, Tunisia.

Yanga ni moja ya timu zinazoshiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo Aprili 20, mwaka huu watacheza ugenini dhidi ya miamba ya soka barani Afrika Al Ahly ya Misri, ambao waliibana na kutoka sare katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles