23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yamsaini ‘mdogo wake’ Drogba

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Klabu ya Azam imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kunasa saini ya straika wa kimataifa kutoka nchini Ivory Coast, Daly Ella Richard Djodi (29), kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Djodi ametokea katika klabu ya Ashantgold FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ivory Coast.

Akizungumzia usajili huo Ofisa Habari wa Azam, Jaffary Iddy amesema kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Afrika Mashariki na Kati kilikuwa kimepwaya katika nafasi za mastraika hivyo ujio wa Djodi utakiimarisha kikosi chao.

“Tunapoenda dakika za mwisho za usajili msimu huu tumeongeza usajili straika wa kimataifa ambaye anatokea nchini Ivory Coast na huyu ndiyo mchezaji wa mwisho wa nje kusajiliwa msimu huu.

“Ni kijana mdogo mwenye nguvu na uwezo mkubwa na amecheza vilabu mbalimbali kabla hajaja Azam ni matumaini yetu kuwa mwalimu ataimarisha kikosi chake upande wa ushambuliaji na niseme tu kwamba tutakuwa tumefunga rasmi dirisha la ushambuliaji,” amesema Iddy.

Aidha kabla Djodi kujiunga na Azama amevitumikia vilabu kadhaa kama Hire FC, Horoya AC, AC Leopards na Stella Club

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles