27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Azam kufa kupona dhidi ya Bandari

Mwandishi Wetu

Timu ya Azam FC kesho itashuka dimbani kumenyana na Bandari FC ya Mombasa nchini Kenya katika michuano ya Kombe la Kagame ambapo mchezo huo ndiyo utaamua kama timu hiyo itafuzu kuingia hatua ya robo fainali.

Katika mchezo wao wa mwisho na KCCA ya Uganda, Azam ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Akizungumza na Mtanzania Digital akiwa nchini Rwanda, Ofisa Habari wa timu hiyo Jaffar Iddy amesema timu hiyo imejianda vya kutosha na ili wasonge katika hatua inayofuata ya robo fainali wanahitaji ushindi au sare.

“Tuko vizuri na leo umefanya mazoezi ya mwisho, mchezo wetu wa kesho na Bandari ndiyo karata yetu ya mwisho ni mchezo ambao tunahitaji ushindi ili tuweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali katika mashindano haya.

“Wachezaji wote wako salama hakuna majeruhi, kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo wa kesho na timu imejipanga vizuri na wachezaji wana hari kubwa ya kupambana kesho, tunahitaji sare au tushinde ili tuweze kusonga mbele na tunasubiri kwa hamu kubwa mchezo wa kesho.

“Nyumbani huko Tanzania mtuombee Azam iko hapa inawakilisha nchi lakini pia kama mabingwa watetezi tunahitaji kombe turejee nalo nyumbani,” amesema Iddy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles