24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Azaki zatakiwa kuielezea jamii ripoti ya CAG

SHEILA KATIKULA ,MWANZA

MRATIBU wa Asasi za Kiraia (AZAKI) Manispaa ya Ilemela ,Yusuph Omollo  amezitaka asasi hizo kuielezea jamii ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) bila kujihusisha na siasa.

Hayo yalisemwa juzi wakati  akimwakilisha Ofisa Maendeleo wa Mkoa wa Mwanza kwenye jukwaa la wakurugenzi wa Azaki kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa lililoandaliwa na Shirika la Kutetea wafanyakazi wa nyumbani la Wotesawa kwa kushirikiana, Wajibu na Foundation for civil Society.

Omollo alizitaka asasi kutojihusisha na siasa katika kuwaelimisha wananchi kuhusu kutambua ripoti hiyo ili waweze kupata uelewa.

“Baada ya kuifahamu ripoti hii kila mtu ana wajibu wa kwenda kwenye jamii kuelimisha  ili waweze kuitambua vizuri na kuifanyia kazi  kwani kuna baadhi ya wananchi wa vijijini hawanauelewa,” alisema Omollo.

Akizungumzia ripoti ya CAG ya mwaka 2017/2018, CAG mstaafu, Ludovick Utouh alisema ni vyema Serikali ni vema kusimamia utekelezaji wa muongozo wa usimamiaji wa viashiria vya rushwa udanganyifu na ubasilifu kwani rushwa ni adui wa haki.
Aliongeza kuwa bunge na ofisi ya CAG kufanyia kazi ripoti zake kwani  kuna umuhimu wa ofisi hizo kuelewana kwa mustakabali wa nchi sanjari na kuiomba Serikali kuzingatia makubaliano ya mkataba katika utoaji wa fedha za miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga alisema  azaki za kirahia zinakaguliwa kila mwaka na wadau wao wote lazima wakaguliwe kama moja ya kigezo chakuendelea kufanya kazi na Azaki zinazopata ruzuku kutoka kwao.

Kabadi Ngika kutoka Shirika la kuwainua wakulima(FEI)alisema, azaki zishirikishwe kwenye kuingia kwenye vikao mbalimbali hasa kwenye mabaraza ya madiwani ili wawe na uelewa juu ya mgawanyo wa fedha na bajeti zinazopangwa ndipo itakuwa na uwezo wa kusimamia na kutoa elimu kwa jamii kuliko kusubiri ripoti ya CAG

Naye Ofisa utetezi wa WoteSawa, Veronica Lodrick alisema wameamua kuandaa jukwaa la wakurugenzi wa Azaki ili wapate kueleweshwa ripoti ya CAG nao wakaelimishe jamii ili waisukume serikali kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na CAG kwenye ripoti yake ya 2017/2018.
 Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Afya ni Mtaji Tanzania (EAHP), Edna Matasha aliyashukru mashilika hayo kwa kuanaanda mkutano huo wenye lengo la kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu ripoti  za CAG kupitia Azaki  hizo ili kukuza uwajibikaji na utawala bora nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles