29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wasweden wanusurika kwenda jela

NA KULWA MZEE
DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Kampuni ya Biabana,  Anna Kristina Edler, (54) na mumewe Anders Svensson (58)  wamenusurika kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela, baada ya kufanukiwa kulipa faini ya Sh milioni 20.

Wawili hao walihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na nusu au kulipa faini ya Sh milioni 20 kwa kosa la kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi nchini bila kibali cha Uhamiaji.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , Huruma Shaidi leo Juni 3,2019.

Washtakiwa hao raia wa Sweden walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na  kibali.

Baada ya kusomewa mashtaka  yao, washtakiwa wamekiri makosa na wamehukumiwa kulipa faini ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani. Hata hivyo lmelipa faini.

Wakili wa Serikali, Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka jana na Aprili 3, 2019 maeneo ya Mikocheni, mshtakiwa Elder,  akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi  katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara ya Uhamiaji.

Katika shtaka la pili imedaiwa,  mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa Kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idaravya Uhamiaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles