27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jamhuri yakwama kesi ya mhasibu Takukuru

NA KULWA MZEE
DAR ES SALAAM

KESI inayomkabili Mhasibu Mkuu wa zamani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake imekwama kuendelea kwa kuwa mashahidi watano waliotoa ushahidi hawajalipwa stahiki zao.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa amedai hayo leo asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotakiwa kuendelea na ushahidi.

Mbagwa amedai  kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri lakini wameshindwa kuwaita mashahidi wengine kwa sababu shahidi wa 9,10,11,12 na 13 ambao tayari walishatoa ushahidi hawajalipwa stahiki zao.

“Kutokana na hali hiyo mheshimiwa tunaomba mahakama itoe amri kwa uongozi wa Mahakama ili waweze kuwalipa mashahidi stahiki zao,” alidai.

Hakimu Simba alisema watalitatua tatizo hilo kwa kuwa kesi hiyo ni ya muda mrefu na walikubaliana waletwe mashahidi ili kesi imalizike.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Juni 17 kwa kutajwa na itaendelea kusikilizwa Juni 18, 20 na 24, upande wa Jamhuri umeelekezwa kuleta mashahidi.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles