20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

AUSSEMS, NDAYIRAGIJE wanyukana nje ya uwanja

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM 

ZIKIWA zimesalia siku mbili kabla ya pambano lao, kocha wa Simba, Patrick Aussems na kocha wa Azam, Etienne Ndayiragije wameendelea kutambiana kila mmoja akisema ataibuka na ushindi  timu zao zitakapouamana.

Timu hizo zitashuka dimbani kuumana kesho kutwa katika mchezo wa wa Ngao ya Jamii, kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa  Uwanja wa Taifa,  Dar es Salaam.

Simba ndiye bingwa mtetezi wa Ngao ya Jamii, baada ya msimu uliopita kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,  Mwanza.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems  alisema anafahamu Azam ina kocha mpya pamoja na baadhi ya wachezaji wapya kusudio lao ni kuanza msimu vizuri kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.,

“Tunaendelea na mazoezi huku nikiyafanyia kazi baadhi ya mapungufu, mchezo na Azam utakuwa ni mgumu lakini mipango yetu ni kuanza msimu mpya kwa kuwafunga Azam na kubeba kikombe,” alisema.

Alisema atafuatilia  kwa karibu michezo ya wapinzani wake hao katika michuano ya Kombe la Kagame ili kutafuta mbinu za  kuwakabili na kuwashinda.

“Bado nitaendelea kuwakosa wachezaji wangu waliokuwa majeruhi ambao ni Ibrahim Ajib, Aishi Manula na Wilker Henrique Da Silva, hadi pale hali zao zitakapoimarika,” alisema.

Lakini Kocha wa Azam, Etienne Ndayiragije amejinadi kuwa kama aliweza kuwamudu Wekundu hao akiwa na kikosi cha thamani ya kawaida cha Mbao, hana shaka kwamba atawafunga mdogo akiwa na kikosi imara cha Azam Complex.

“Ninaifahamu Simba vizuri sana kwakua nimekutana nayo nikiwa na Mbao pia KMC, sina shaka kwamba Azam ina kikosi imara cha kuwamudu na kupata ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles