23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Mwanri aagiza watumishi Tabora kukatwa mishahara

Mwandishi wetu-Tabora

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kuwakata mishahara watumishi wote wa mkoa huo wanaodaiwa masurufi yaliyosababisha hoja ya kiukaguzi ya Sh milioni 4.7 katika ripoti ya Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Agizo hilo alilitoa jana wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya mbalimbali  kutoka ripoti ya ukaguzi ya CAG kwa mwaka 2017/18.

Alisema ndani ya wiki watumishi wote wanaodaiwa wahakikishe wamelipa fedha hizo au wakatwe kwenye mishahara yao.

Mwanri alisema wasipo katwa fedha hizo hoja hiyo itaendelea kujitokeza na kuchafua hesabu za Manispaa ya Tabora.

Sanjari na hilo Mwanri huyo ametoa wiki mbilli kwa wakuu wa Idara kuhakikisha wamefanyia kazi hoja zote za CAG na kuwalisilisha vielelezo ili ziweze kufungwa.

Alisema mkuu wa idara ambaye ndani ya kipindi hicho hatashindwa kujibu hoja hizo na kusababisha kuendelea kuwepo atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika nafasi yake.

Mwanri alisema hoja zigawanywe katika Wakuu wa Idara mbalimbali ili waanze kuzifanyika kazi mapema.

Ameutaka pia uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanakusanya madeni yote ya ardhi na mikopo ya wanawake, vijana na walemavu zaidi ya milioni 536.

Alisema eneo la kwanza linatokana na mauzo viwanja ambapo waliotakiwa kufidiwa maeneo yao hawakulipwa na wale ambao walipewa viwanja wamekuwa wakilipa kidogo dogo na kusababisha deni kufikia Sh milioni 503.

Mwanri alisema ni vema wakakaa chini na kushughulikia tatizo hilo ili hoja hiyo iweze kufutwa na kuondolewa katika vitabu vya CAG.

Kwa upande wa mikopo iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake na vijana ipatayo shilingi milioni 33.7 ambayo haijarejeshwa.

Alisema ni vema fedha hizo vikundi hivyo vifuatiliwe na virudishe mikopo hiyo kwa ajili ya kutoa katika vikundi vingine.

Aidha Mkuu huyo Mkoa amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora kuonyesha mpango wa kulipa madeni mbalimbali ambayo wanadaiwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa kuwachukulia hatua watumishi wote ambao wameisababishia Halmashauri hiyo kuzalisha hoja za kiukaguzi.

Alisema watumishi ni vema wakajitahidi kuzuia hoja na zio kutoa maamuzi ambayo yanasababisha kuendelea kuzalisha hoja kila mwaka .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles