28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Aunt Ezekiel: Nina haki ya kuhama chama

anty ezakielMWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka chama kimoja na kwenda chama kingine.

Licha ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama chama hicho na kujiunga na kingine
kutokana na kukubali sera za chama hicho.
“Sera za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala sijapokea fedha wala gari kuhamia
huko kama inavyosemekana, bali nafsi na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.
“Nashangaa maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia kama walivyo wengine,
umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda yanayoaminika kuwa jezi ya chama alichokihama

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles