23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

K.O awasifi a Nahreel, Diamond

KOJULIET MORI (TUDARCO)

RAPA wa Afrika Kusini, Ntokozo Mdluli, ‘K.O’ amewamwagia sifa nyingi prodyuza, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ na msanii wa kiwango cha juu, Abdul Nassib ‘Diamond Platinum’ kwa kazi zao nzuri zinazofanya vizuri nje ya Tanzania.

Rapa huyo aliweka wazi mapenzi yake kwa wasanii hao akiwa katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania, akitembelea vituo mbalimbali vya redio na televisheni pamoja na kukutana na wadau wa muziki nchini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Akiwa katika mahojiano na vituo mbalimbali vya redio, K.O alisikika akiwanadi wasanii hao huku akieleza tamaa yake ya kufanya kazi na prodyuza Nahreel, ambaye hata hivyo wameshaanza utaratibu wa kurekodi wimbo wa pamoja na prodyuza huyo kwa kumshirikisha mkali wa hip hop nchini, Joh Makini.

Hata hivyo, K.O alisisitiza kwamba amepokea beat kadhaa kutoka kwa prodyuza huyo anazotaraji kuzifanyia kazi akiwa na msanii mwenzake nchini humo, A.K.A, ambapo anadai nyimbo hizo zitakuwa katika albamu yake ijayo. “Beat zake hazisikiki kama za Afrika Kusini au Marekani, bali zinasikika vizuri na special ambazo hazipatikani kokote

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles