MWANAMUME mmoja mwenye umri wa miaka 26, amekufa kwa kupigwa na radi huku wake zake wawili wakijeruhiwa, wakati wa mvua kubwa iliyonyesha wilayani Laela katika Mkoa wa Rukwa, anaripoti Ibrahim Yassin.
Mwanamume huyo na wake zake walikuwa wakirejea nyumbani kutoka shambani.
Tukio hilo lilitokea juzi katika Kitongoji cha Nakanga Kijiji cha Nkima Kata ya Mpui.
Mke mkubwa wa wa mwanamume huyo, Huruma Mwananjera, ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo alisema mume wao alipatwa na mauti papo hapo huku wao wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini wakiwa hawajitambui.