30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

AUAWA KWA RADI

MWANAMUME mmoja  mwenye umri wa miaka 26, amekufa kwa kupigwa na radi huku wake zake wawili wakijeruhiwa, wakati wa mvua kubwa  iliyonyesha  wilayani Laela  katika Mkoa wa Rukwa, anaripoti Ibrahim Yassin.

Mwanamume huyo na wake zake  walikuwa   wakirejea nyumbani kutoka shambani.

Tukio  hilo  lilitokea  juzi katika Kitongoji cha Nakanga Kijiji cha Nkima Kata ya Mpui. 

Mke mkubwa wa wa mwanamume huyo, Huruma Mwananjera, ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo alisema mume wao alipatwa na mauti papo hapo huku wao wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini wakiwa hawajitambui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles