23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZAZI WAAJIRI MWALIMU WA HESABU, WAMLIPA MSHAHARA

NA BEATRICE MOSSES


UKOSEFU wa walimu wa   hesabu umewafanya   wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Sekondari Bagara  wilayani Babati  kuunda kamati ya kuboreshai  taaluma shuleni hapo.

Katibu  wa Kamati hiyo, Dismas  Kokumo  alipozungumza  na MTANZANIA juzi  alisema wazazi wamekubaliana  kuchanga Sh 25,000 kila mmoja kwa ajili ya kumlipa mwalimu wa somo hilo.

Alisema vilevile wamekubaliana kutoa Sh 5,000 kila mmoja kwa mwaka kwa ajili ya kununu karatasi.

“Baada ya kuona kuna tatizo la walimu wa   hesabu tulikubaliana   wazazi tuchangie Sh 25,000  kwa ajili ya  kumlipa mwalimu kwa mwaka kila mwanafunzi na Sh 5000 za

  karatasi,’’ alisema  Kokumo.

Alisema  wameweka utaratibu wa  wanafunzi kupewa mazoezi  na mwalimu huyo kujua kama    wanachofundishwa wanakielewa .

Kokumo alisema  kamati iliyochaguliwa na wazazi  ndiyo inaratibu suala la kumlipa mwalimu baada ya michango kuchangwa na fedha kuhifadhiwa katika Benki ya CRDB.

“Kupatikana kwa mwalimu wa hesabu kumesaidia  kuongeza ufaulu katika shule hii maana  tumetoka  zero 80  mwaka uliopita hadi  zero tano ambazo  ni za wale watoro,’’ alisema.

Naye Mkuu wa Shule hiyo, Emmanuel Dahaye,    alikiri wanafunzi kuchangishwa michango kwa ajili ya mwalimu wa hesabu   baada ya   uamuzi wa wazazi.

Alisema  kufanya hivyo kulitokana na  waraka wa elimu uliotolewa na  TAMISEMI  uliowataka kufanya hivyo inapobidi baada ya kukubaliana na wazazi.

"Ni nyaraka ambazo tulipewa kwamba  shule inapokuwa na tatizo fulani wazazi wenyewe wafanye uamuzi, wafanye mchanganuo na hizo shughuli zote ziratibiwe na wazazi wenyewe," alisema  Dahaye.

Alisema baada ya kukubaliana waliamua kila mwanafunzi  achangie Sh 12,500 kwa muhula  mmoja lakini hata ambao hawachangii kwa wakati   hawawafukuzwi  bali wanavumiliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles