Nairobi, Kenya
Umoja wa Afrika umezitaka Somalia na Kenya kufanya mazungumzo ili kupunguza mvutano wa mpakani uliosababisha vifo vya watu 11 na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumatatu.
Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ambapo amezitaka nchi hizo jirani kusitisha uhasama na kufanya mazungumzo kwa mujibu wa mchakato unaoongozwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali za Afrika Mashariki (IGAD), ili kutatu migongano kati yao.
Mahamat amesema, amani ya mpaka kati ya Somalia na Kenya ni muhimu sana kwa utulivu wa kikanda.