33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaotupa dawa kiholela majumbani waonywa

Aveline Kitomary, Mwanza

Kutokana na madhara makubwa yanayoweza kutokea ya utupaji dawa kiholela, Mamlaka ya Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi(TMDA) Kanda ya Ziwa imetoa wito kwa jamii kuacha kutupa dawa hovyo ili kuepuka madhara ya kiafya na kimazingira.

Mkaguzi wa Dawa wa Mamlaka hiyo kwa Ukanda wa Kanda ya Ziwa, Mtani Njegere amesema kuwa ni vyema dawa zinazotumika majumbani kurejeshwa katika maeneo yanayotoa huduma za tiba ili mamlaka husika zizifikie na kuteketezwa kwa njia salama.

Mkaguzi wa Dawa wa Mamlaka TMDA kwa Ukanda wa Kanda ya Ziwa, Mtani Njegere

Njegere amesema hayo wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika maabara ya TMDA iliyoko jijini Mwanza.

“Kuna dawa ambazo ziko majumbani mtu anaweza kutumia akishapona anaziacha na kuzitupa ovyo natoa rai kwamba wakati wanapokuwa na mabaki ya dawa wawasiliane na maeneo ambayo yanatoa huduma za tiba kama famasi wazirudishe.

“Wao wawasiliane na sisi ili wakati wa uteketezaji wa dawa walizonazo tutazikuta kwa sababu kutupa dawa kwenye mazingira au kwenye maji au eneo lolote inaathari kubwa kwa wanadamu, wanyama na mazingira,” amesema Njegere.

Amesema ni vyema mgonjwa akipewa dawa atumie kama alivyoelekezwa na daktari kwa kukamilisha dozi inayotakiwa.

Jengo la TMDA Kanda ya Ziwa

Akizungumzia namna ya uteketezaji wa dawa Njegere amesema dawa na vifaa tiba huteketezwa baada ya kukosa sifa.

“Baadhi ya dawa zinaweza kubainika kwenye soko kuwa ni dawa bandia lakini pia kuna zile ambazo hazikidhi mahitaji ya kutibu magonjwa na vifaa tiba au uhifadhi mbaya, kwani karibu dawa zote zinamasharti ya kuhifadhi.

“Uteketezaji wa dawa na vifaa tiba uko wa aina mbili kuna uteketezaji wa hiari kutoka kwa wafanyabiashara na uteketezaji usio wa hiari, bidhaa ambazo zinateketezwa bila hiari tunafanya ukaguzi sehemu mbalimbali na tunaweza kubaini kuwa zipo dawa hazikidhi viwango hizi zinaweza kuwa zimehifadhiwa vibaya au dawa bandi au sababu zozote,” amebainisha.

Njegere amesema kila uteketezaji wanaoufanya unazingatia sheria zilizowekwa pamoja na kufata hatua zinazotakiwa.

“Hatua mbalimbali ni kama mfanyabiashara kufanya maombi ya kuhitaji kuteketeza hatua hiyo huambatana na dawa au vifaa tiba vinavyohitaji kuteketezwa na orodha inakuwa na taarifa muhimu kama jina la biashara ya dawa, jina halisi la dawa, nguvu ya dawa, toleo la dawa, tarehe ya kuisha muda wa matumizi,aina ya dozi, kiasi cha dawa, thamani ya dawa na sababu ya kuteketeza.

“Kutokana na kukua kwa teknolojia maombi yanaweza kufanyika kwa njia ya mtandao baada ya kuwalisilishwa wakaguzi huandaa kuthibitisha taarifa ya vitu vilivyowasilishwa na vitu vilivyowasilishwa, ,wakaguzi pia hupendekeza njia bora ya uteketezaji wa dawa kutokana na aina ya dawa.

“Ukaguzi wa kuridhisha hufanyika na taarifa zote hujazwa katika fomu (verification form) ili wafanyabiashara wasio waaminifu wasiweze kudanganya thamani ya dawa mfano dawa ni Sh milioni 15 lakini atakuambia Sh milioni na mwisho tunatoa cheti cha uteketezaji,” amesema Njegere.

Ameeleza kuwa iwapo bidhaa zitadhibitishwa pamoja na thamani mamlaka huamua mahali ambapo bidhaa zitatekewzwa na kumtaarifu mfanyabiasha kwa barua pia taarifa zitatolewa kwa mamlaka ya usimamizi wa eneo ambalo uteketezaji utafanyika ili kukamilisha zoezi.

“Mamlaka huwajibika kuzitaarifu mamalaka zingine ambazo zinashiriki katika zoezi la uteketezaji akiwemo mwakilishi wa mmiliki wa dawa, utekezaji unazingatia sheria iliyopo pamoja na mwongozo wa uteketezaji dawa nchini mamalaka pia huzingatia sheria ya baraza la mazingira nchini.

“Tunazingatia njia sahihi ya uteketezaji ili kukamilika na bidhaa zimeharibika kwa asilimia 100, kuhakikisha kuwa havina tena madhara kwa mazingira na viumbe,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles