27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

ASKOFU NZIGILWA AWATAKA WAUMINI KUACHA MALUMBANO WAIONE PEPO

Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam


Askofu Msaidizi wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa amewataka waumini kuwa na moyo wa huruma hasa katika kipindi hiki cha kukumbuka mateso ya Yesu Kristo na kuondoa malumbano ili waweze kuiona pepo.

Akihubiri katika misa ya Ijumaa Kuu leo Machi 30, iliyofanyika katika Kanisa ka Bikira Maria Mama wa Huruma, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amesema wawe tayari kusamehe kwa wote waliowakosea na kuondoa visasi na vinyongo ambavyo vinaweza kuharibu maisha yao.

“Katika kipindi hiki cha kukumbuka mateso ya Yesu Kristo, tunapaswa kukumbuka matendo ya huruma ambayo yatazidi kutuongezea imani na kuondoa visasi na malumbano katika jamii na familia zetu.

“Wakristo tunatakiwa kujifunza kukaa kimya na kuepusha maneno na kumgeukia Kristo ili uweze kumueleza shida zako, jambo ambalo linaweza kukusaidia ukaikuta huruma yake.

“Kila mmoja anapomuangalia Yesu msalabani anapaswa kusema yesu dhambi zangu zimekuhukumu kwa sababu alikuhumiwa katika mazingira ya uonevu,” amesema.

Aidha, Askofu Nzigilwa amesema watu wanapaswa kumuonea huruma mtu anayeteseka na kamwe hawashiriki kwa ajili ya kusababisha mateso Kwa mwingine na kwamba kila mmoja anapaswa kuweka azimio la kuwa mtetezi kwa wanaoonewa na kamwe wasinyanyase mtu au kumtendea mabaya.

“Kila binadamu anateseka kwa namna tofauti ili kupimwa imani yake kama ipo imara, hivyo basi wanapaswa kuwa wavumilivu wa moyo na kumkimbilia Mungu ili iwe sehemu ya ukombozi,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles