ASKOFU MALASUSA: MSIFANYE MAMBO KWA KUFUATA MAKUNDI

0
858

Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam


Askofu wa Kanisa la Kiinjili Kiluteri Tanzania (KKKT), Dayosisi na Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, amewataka waumini wa kanisa hilo kujipambanua kwa kufahamu mema na mabaya badala ya kufuata na kufanya mambo kwa kufuata kinachosemwa na makundi ya watu.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Machi 30, katika Ibada takatifu ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front,  jijini Dar es Salaam.

Dk. Malasusa amesema hata kifo cha Yesu Kristo kilitokana na Pilato kusikiliza kundi kubwa la watu waliotaka asulubiwe.

“Watu wengi hufanya maamuzi kwa kufuata makundi ya watu yanasema nini, kwa hiyo hata kifo cha Yesu Kristo kiliharakishwa na kundi la watu waliopiga kelele asulubiwe na kuwachanganya viongozi.

“Hivyo ndivyo tunavyoishi leo kwa kufuata makundi ya watu, kwa hiyo lazima wakristo tujipambanue. Ijumaa Kuu ni zaidi ya kuvaa nguo nyeusi na kutokula baadhi ya chakula,” amesema Askofu Malasusa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here