27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Askari Zimamoto kizimbani kwa tuhuma za mauaji

AVELINE KITOMARY NA ERICK MUGISHA (DSJ) – DAR ES SALAAM

WATU wawili akiwamo askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam na kusomewa shtaka la mauaji.

Waliofikishwa kizimbani ni Jackson Michael (37) ambaye ni askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mkazi wa Zinga,  Bagamoyo mkoani Pwani na Itagala John (24) mkazi wa Tabata Bima, Dar es Salaam.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Frank Moshi, Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Abudi Yusuph, alidai mnamo Aprili 24,  mwaka huu eneo la Bunju A, Wilaya ya Kinondoni washtakiwa walimuua Gaspar James.

Hakimu Moshi alisema washtakiwa hawatakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Mwendesha mashtaka wa Jamhuri alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kukamilishwa kutajwa.

Kutokana na shtaka  hilo kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria, washtakiwa walirudishwa rumande hadi Julai 15, mwaka huu shauri hilo litakaposikilizwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles