26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Gondwe: soko la muhogo nchini litachuana na Cambodia, Thailand

Amina Omari, Handeni

Zao la Muhogo linalolimwa wilayani Handeni mkoani Tanga, soko lake litachuana na nchi za nje zinazolima kwa wingi zao hilo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wa wilaya hiyo, Godwin Gondwe wakati Mwenge wa Uhuru ulipokagua shamba la mfano la zao hilo lililopo katika kata ya Mkata.

Amesema ubora wa zao hilo unaozalishwa wilayani humo hauna tofauti na unaozalishwa katika nchi za Cambodia, Thailand na Vietnam.

 “Kutokana na ubora wa mihogo yetu ndiyo maana kwa mwaka huu tayari makampuni matatu ya nchini China tayari yameshakuja na kuonyesha nia ya kununua muhogo mkavu kutoka kwa wakulima wilayani kwetu,” amesema Gondwe.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally alisema ili kufikia Tanzania ya viwanda ni lazima tuongeze kasi ya uzalishaji wa malighafi zitakazotumika katika viwanda hivyo.

“Ni vema kuja na mikakati madhubuti ya kuhakikisha zao hilo linachakatwa lote bila ya kutupa kitu ili wakulima wetu waweze kunufaika kiuchumi na serikali kupata mapato yake,” amesisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles