25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Askari Senapa lawamani Serengeti

NA MALIMA LUBASHA -SERENGETI 

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara limewalalamikia askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) kwa kukamata mifugo ya wananchi, kuwalipisha faini kubwa kisha kuhukumiwa kifungo jela.

Hali hiyo imesababisha uhusiano mzuri kati ya wananchi wanaopakana na Senapa kulegalega jambo linaloelezwa kuhatarisha jitihada za uhifadhi wanyamapori zinazochulikuwa kulinda rasilimali hiyo.

Hoja hiyo iliibuliwa mjini hapa juzi na Diwani wa Kata ya Mbalibali, John Ng’oina, alipowasilisha taarifa ya kata ya robo tatu ya ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Januari hadi Machi, mwaka huu katika kikao cha baraza hilo.

Ng’oina alisema askari hao wanakamata mifugo hiyo kwa madai ya kuingia hifadhini kinyume cha sheria.

Alisema walinzi wa rasilimali hiyo ni wananchi wenyewe, ndiyo maana Tanapa walianzisha Kitengo cha Ujirani Mwema mwaka 1985 lengo likiwa ni kuwataka  wananchi hao kuwalinda wanyama pori, kuendeleza uhusiano kwa kuwajengea uwezo kufahamu umuhimu wa uhifadhi na kudhibiti vitendo vya ujangili huku wakichangia miradi vijijini katika sekta za elimu, afya na maji.

Pia madiwani wengine waliwalalamikia askari hao kwa kukamata mifugo na walisema ipo haja ya kukutana na uongozi wa Senapa kujadili changamoto hiyo ili kuondoa tofauti hizo.

Naye Diwani wa Kata ya Nagusi, Jackson Manyeresa, aliwalalamikia askari wanyamapori wa Grumeti Reserves kuwa wanavamia kaya na kufanya upekuzi na kuwafanya wananchi kuwa na hofu.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, alisema ataitisha kikao kati ya madiwani na mhifadhi mkuu wa Senapa kujadiliana juu ya changamoto hiyo ili kukomesha tabia ya wananchi kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi kutafuta malisho huku wakijua hilo ni kosa kisheria.

Aliwataka wananchi wa vijiji vyote wanaoishi kando ya hifadhi na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo kuacha tabia ya kuingiza mifugo yao hifadhini na alishauri endapo wataingiza ng’ombe hifadhini askari hao wanatakiwa kuwaonya na si kuwakamata kama ilivyo sasa na endapo watarudia ndipo wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles