20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Suma JKT yatakiwa kukamilisha ujenzi jengo la Uhamiaji

Na Mwandishi Wetu -MOHA

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT) kujenga jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kwa ufanisi mkubwa na akabidhiwe baada ya miezi 18. 

Akizungumza jijini hapa jana kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa jengo hilo, kati ya wizara hiyo na Suma JKT iliyoongozwa na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu, alisema hana shaka na uwezo wa mkandarasi huyo na anaamini ujenzi huo utakuwa bora na utakamilika kwa wakati.

“Baada ya maandalizi ya ujenzi huu kuchukua muda mrefu, lakini hatimaye tumekamilisha, hivyo nawaomba ndugu zangu tufanye kazi vizuri kabisa, na leo (jana) ndiyo siku ya kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi huu,” alisema Kingu. 

Alisema watafuatilia kwa karibu ujenzi huo na ambao mkandarasi ni Suma JKT na mshauri elekezi ni Chuo Kikuu cha Ardhi na anatarajia jengo hilo litakuwa bora zaidi kutokana na uwepo wa wadau hao.

Kwa upande wake, Busungu aliishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuwa na imani na Suma JKT na kuipa kazi ya ujenzi wa jengo hilo.

“Tunaishukuru wizara kwa kutupa kazi hii ya ujenzi wa jengo hili ambalo ni la ghorofa nane, tunaahidi kulikamilisha baada ya miezi 18, na tutapiga kazi kadiri inawezekana, tupo tayari kwa kazi yenye uweledi wa kuzingatia muda na ubora ambao utawauza zaidi Suma JKT,” alisema Busungu.  

Mkataba huo ulisainiwa na viongozi hao huku ukishuhudiwa na wanasheria wa taasisi hizo ambao ni Mkurugenzi wa Sheria wa wizara hiyo, Marlin Komba na Kapteni Joyce Mwaikofu kutoka JKT. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles