Asilimia 96 ya wanawake hudhalilishwa sokoni

0
733

dsc_0645

Na MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM

ASILIMIA 96 ya wanawake wanapitia ukatili wa kijinsia katika masoko ya Manispaa ya Ilala na Temeke, Dar es Salaam.

Aidha, kikundi cha wahuni kinachofahamika kwa jina la Mashabanga, kimetajwa kuhusika na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake wanaofanya biashara katika soko la Mchikichini wilayani Ilala.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye masoko, Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa, alisema kikundi hicho kinaongoza kwa kufanya vitendo hivyo, na matumizi ya dawa za kulevya.

“Hili suala limekuwa tatizo kubwa si soko hili tu na mengine, kuna vijana hawana uadilifu, walevi wa dawa za kulevya na bangi, waliofikia hatua hata kuwadhalilisha wanawake kwa kuwafanyia ngono huku kwenye vibanda vya kuuzia nguo.

“Tulishawafuatilia na kuwakamata vijana hao ambao uhamisha tabia hizo kwenye masoko mengine, lakini cha kusikitisha wafanyabiashara wanawatetea na kuwadhamini polisi, wakidai ni vijana wao wa kufanyia biashara zao,” alisema Ngowa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here