24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyetesa ‘house girl’ afungwa miaka 2

b897c623

Na MANENO SELANYIKA–DAR ES SALAAM

MKAZI wa Mwananyamala kwa Manjunju, Dar es Salaam, Amina Maige, amehukumiwa kwenda jela miaka miwili na kulipa faini ya Sh 500,000 baada ya kupatikana na hatia ya kumtesa, kumjeruhi aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani, Yuster Kashinde.

Mshtakiwa pia amepewa adhabu ya kumlipa mlalamikaji Sh milioni mbili  kama gharama alizotumia mlalamikaji kutibiwa maumivu ya vidonda alivyomsababishia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Caroline Kiliwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni hiyo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa mahakamni hapo na upande wa mashtaka.

“Kwa mazingira hayo Mahakama hii inakutia hatiani kwa kosa hilo kutokana na ushahidi wa kina uliowasilishwa hapa na   mashahidi wanane wa upande wa mlalamikaji,” alisema Kiliwa.

Hakimu alisema shahidi namba moja ambaye ni Yuster aliiambia mahakama kwamba majeraha aliyoyapata   yalisababishwa na mshtakiwa.

Alisema mahakama ilithibitisha majeraha hasa sehemu ya sikio la kushoto ambalo liliharibiwa kabisa.

“Utatumikia kifungo cha nje miaka miwili kwa usimamizi wa maofisa wa ustawi wa jamii hivyo uwe makini.

“Endapo utapatikana na kosa la jinai kabla ya kumaliza kifungo hiki adhabu itabadilika kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Katika utetezi,  Wakili wa Amina, Emmanuel Muga, aliiomba mahakama   isimpatie mteja wake adhabu kali kwa kuwa ni kosa la kwanza na hajawahi kupatikana na shtaka la jinai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles