KIUNGO wa Arsenal, Martin Odegaard, anaamini timu hiyo ina uwezo wa kulinyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya miaka miwili ijayo.
Licha ya Washika Bunduki hao kutoshiriki michuano hiyo tangu mwaka 2017, Odegaard amesema bado wanaweza kufanya vizuri na kurudisha hadhi ya klabu hiyo ya Kaskazini mwa Jiji la London.
“Nafikiri msimu huu tunataka kurudi kwenye mashindano ya Ulaya. Baadaye, tutachukua mataji, Ligi ya Mabingwa na hatimaye Ligi Kuu miaka michache ijayo,” amesema.
Odegaard raia wa Norway, alisajiliwa moja kwa moja na Arsenal akitokea Real Madrid, amecheza mechi 23 na kufunga mabao mawili na ‘asisti’ tatu.