27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Arsenal, Man City katika vita ya kibabe leo

LONDON, England

KIKOSI cha Arsenal leo kitashuka dimbani kuikaribisha Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.

Arsenal itaingia uwanjani ikitoka kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham katika mchezo wao wa ligi uliopita, , ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha wa muda wa timu hiyo, Freddie Ljungberg.

Ushindi huo ulikuja baada ya timu hiyo kucheza mechi tisa mfululizo bila kuvuna pointi tatu, kabla ya kurejea kwenye reli katika mchezo wao uliopita wa wakiwachapa Wagonga Nyundo hao wa jiji la London.

Man City itakuwa ikihizitaji pointi tatu kwa hali na mali ili kupunguza pengo la pointi 14 kati yao na Liverpool wanaoongoza katika msimamo wa ligi hiyo.

City itaingia uwanjani ikiwa na hasira baada ya kupoteza mechi yao ya mwisho ya ligi kwa kuchapwa na watani zao, Manchester United mabao 2-1, hata hivyo ilirejesha hali ya kujiamini baada ya kuitandika Dynamo mabao 4-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki.

Msimu uliopita, Arsenal ilipoteza mechi zote mbili ikianza kucharazwa mabao 2-0 pale Emirates, kabla ya kwenda kushindiliwa 3-1 walipozikanyaga nyasi za Uwanja wa Etihad.

Mara ya mwisho, timu hizo zilikutana Februari, mwaka huu na Arsenal ilikubali kichapo cha  mabao 3-1.

Licha ya Arsenal kuwa nyumbani, lakini ukweli ni kwamba rekodi haziwabebi kwani hawajashinda katika mechi zote tano walizocheza Emirates katika kipindi cha hivi karibuni.

Arsenal itawakosa Dani Ceballos, Rob Holding, Granit Xhaka na Kieran Tierney wanaouguza majeraha, huku pia kukiwa na kuwakosa Héctor Bellerin na Nicolas Pepe.

Man City wao, watawakosa Leroy Sane, Aymeric Laporte, Sergio Aguero na John Stones, huku pia David Silva na Ederson wakiwa shakani.

Rekodi za jumla zinaonyesha kuwa Arsenal inaongoza kwa kuibuka na ushindi katika mechi za ligi walizokutana na Man Cit,ikishinda 23, kupoteza 11 na kutoka sare 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles