24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Boris ndani ya mchakamchaka mwingine tena wa siku 50

LONDON, UINGEREZA

SIKU moja baada ya matokeo ya uchaguzi nchini Uingereza kuonyesha ushindi wa kishindo wa chama cha Waziri Mkuu, Boris Johnson cha Conservative, sasa anaanza mchakamchaka wa siku takribani 50 bila kupumzika  kuhakikisha analitoa taifa hilo ndani ya Umoja wa Ulaya (EU).

Kesho Boris anatarajiwa kutangaza mabadiliko kidogo katika serikali yake.

Wabunge watakusanyika Jumanne tayari kwa kuanza utaratibu wa kula viapo, kabla ya Malkia hajafungua rasmi Bunge Alhamisi.

Boris pia ameahidi kuwasilisha tena bungeni muswada wa makubaliano wa kujiondoa EU uliondolewa kabla ya Krisimasi.

Hatua hiyo itashuhudia wabunge wakianza mchakato wa Uingereza kujitoa EU ifikapo Januari 31 2020. 

Mazungumzo kuhusu masuala ya biashara ya baadae na yale ya mahusiano ya usalama yataanza pengine mapema zaidi.

Wakati hayo yakijiri baadhi ya wachambuzi wameeleza hatari ya Uingereza kugawanyika huku Boris mwenyewe akiahidi kutibu kila jeraha kwa kuungana.

Jana Gazeti la Sueddeutsche  la nchini Ujerumani lilizungumzia hatari ya Uingereza kugawanyika katika kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejipatia ushindi wa wazi kabisa kwenye uchaguzi wa taifa lake.

Gazeti hilo la kila siku la Sueddeutsche limeandika “Dira ya uchaguzi inapaswa kuwa ya mashaka makubwa kwa Boris. Kwamba Wascotland na Waireland ya Kaskazini hawajioni kama sehemu ya serikali yake.

Gazeti hilo limeonya kwamba endapo Boris hatachukua mwongozo wa ushirika pamoja na Umoja wa Ulaya, hatakuwa na uwezo wa kupata maridhiano ya ndani ya nchi yake.

Wakati wachambuzi wakiwa na mtazamo huo  saa kadhaa baada ya Boris kusheherekea ushindi huo wa kishindo ambao haujapata kutokea ndani ya miaka 30 pia alielekea England Kaskazini eneo ambalo chama chake kimepata ushindi mkubwa.

Waziri Mkuu huyo alisema anatumaini ushindi wa Conservatives utawafanya kuwa wamoja kuelekea kwenye mjadala wa Brexit.

Chama chake cha Conservative kimejinyakulia viti vya ubunge 365 kati ya hivyo kikiwa kimeongeza viti 47, wakati chama pinzani cha Lobour kikijipatia viti 203 huku kikiwa kimepoteza vingine 59.

Tayari kiongozi wa chama cha Lobour, Jeremy Corbyn  alisema amefanya yote yaliyowezekana kuhakikisha Labour  inaingia madarakani lakini alisema anatarajia kuachia nafasi hiyo anayoishikilia mapema mwakani baada ya mrithi wake kuchaguliwa na chama.

Alisema uchaguzi mkuu ulitekwa na Brexit, suala ambalo Boris alilifanyia kampeni kwa sauti kubwa.

Lakini Helen Goodman wa chama cha Labour ambaye amepoteza kiti cha Bishop Auckland kwa Conservatives, ameiambia Redio 4 ya BBC kwamba sababu kubwa ya kushindwa ni Jeremy Corbyn kutokuwa maarufu kama kiongozi.

Ingawa mbunge wa Labour  wa York Central, Rachel Maskell, alisema wote wanapaswa kuwajibika kwa matokeo hayo na kwamba haamini katika kumlaumu yeyote na kwamba ufumbuzi wa jambo hilo gumu inabidi utafutiwe njia ya rahisi ya kulitatua. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles