ERICK MUGISHA Na NEEMA SIGALIYE (TUDARCo) – DAR ES SALAAM
MKAZI wa Sinza jijini Dar es Salaam, Abubakari Bakari (22), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la ulawiti.
Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Frank Moshi na Mwendesha Mashtaka wa Serikari, Yussuf Aboud, alidai Machi 21 , 2019 eneo la Sinza wilayani Kinondoni, Dar es Salaam alimlawiti mtoto wa miaka 12.
Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo, ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikari, Aboud alisema upelelezi bado ujakamilika.
Hakimu Moshi alisema dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka Serikali za Mtaa na nakala za vitambulisho na kusaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja.
Mshatakiwa huyo alitimiza masharti hayo ya dhamana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba Mosi, mwaka huu.